Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 21:41

Mlipuko wa bomu wauwa saba Somalia


Vikosi vya usalama Somalia katika eneo la tukio Mogadishu, Sept. 28, 2017.

Maafisa usalama nchini Somalia wanasema mlipuko wa bomu la kwenye gari katika mji mkuu Mogadishu umewaua takriban watu saba na kuwajeruhi wengine sita.

Msemaji wa utawala wa Mogadishu Abdifatah Omar Halane ameiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba gari lililipuka Alhamisi karibu na kituo cha basi chenye harakati katika wilaya ya Hamarweyne.

“Kilichotokea ni bomu lililokuwa ndani ya gari lililipua basi dogo na kuua watu saba na wengine sita kujeruhiwa, Halane ameiambia VOA”.

Mashahidi kadhaa wameiambia VOA kwamba waathirika walikuwa ni raia wa Soamlia ambao walikuwa kwenye kituo cha basi na maeneo ya karibu.

Lengo la mlipuko huo bado haliko bayana, lakini walioshuhudia wanasema magari ya majeshi ya usalama ya serikali yalikuwa yanapita wakati mlipuko ulipotokea. Hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG