Mlipuko mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi na kusababisha moto na kuwajeruhi watu kadhaa.
Mlipuko huo umetokea majira ya saa 7.10 mchana kwa saa za Afrika mashariki katika eneo la kati la kibiashara karibu na chuo kikuu cha Mt.Kenya.
Wafanyakazi wa zimamoto na waokozi walifika katika eneo la tukio. Hakukuwa na taarifa za haraka juu ya kile kilichosababisha mlipuko huo.
Kenya imekuwa ikishambuliwa na mifululizo ya mashambulizi ya guruneti ambapo maafisa wanalilaumu kundi la wanamgambo la al-Shabab na washirika wake. Kenya ilipeleka wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na kundi la al-Shabab tangu mwezi Oktoba mwaka jana.