Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 21:25

Mashambulizi ya kujitoa muhanga yaendelea Afghanistan


Maafisa nchini Afghanistan wanasema kwamba mlipuko wa kujitoa mhanga katika jimbo la kati la Parwan mapema leo umeua karibu watu sita na kujeruhi wengine 22.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Sediq Seddiqi, alithibitisha shambulizi hilo katika wilaya ya Siah Gerd kwa kusema karibu waathirika wote walikuwa raia ikijumuisha wanawake.

Alieleza katika mkutano na wanahabari katika mji mkuu Kabul kwamba polisi walimtambua mshambuliaji huyo na kujaribu kumzuia katika kituo cha ukaguzi ndipo akategua bomu.

Hakukuwa na taarifa za haraka za aliyehusika lakini maafisa wa Afghanistan walidai wanamgambo wa Taliban wanahusika na shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG