Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:06

Mlinda amani auwawa, na mwengine kujeruhiwa DRC


Picha ya Maktaba
Picha ya Maktaba

Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Afrika Kusini amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya helikopta yao kushambuliwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jumapili, kwa mujibu wa taasisi yao. 

Helkopta yao ilishika moto majira ya saa tisa alasiri ikiwa safarini mjini Goma, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, ambako ilifanikiwa kutua, msemaji wao aliiambia AFP.

Chanzo cha tukio hilo la helikopta bado hakijajulikana na eneo lake kamili bado halijajulikana, alisema Amadou Ba, msemaji wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO).

Jeshi la Afrika Kusini pia lilithibitisha tukio hilo.

Helikopta ya Oryx iliungua ikiwa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jumapili, Februari 5, 2023," Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini (SANDF) lilisema katika taarifa yake.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kwamba mwanajeshi mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi, huku mwingine akijeruhiwa lakini alifanikiwa kuendelea kuirusha Helkopta hiyo na kutua salama katika uwanja wa Ndege wa Goma.

Jeshi la Afrika Kusini lipo katika harakati ya kuwajulisha wanafamilia wa wanajeshi waliokutwa na tukio hilo la kusikitisha.

Mkuu wa MONUSCO Bintou Keita amelaani vikali shambulio hilo la uwoga dhidi ya helkopta yenye nembo ya Umoja wa Mataifa, akiongeza kuwa mashambulizi dhidi ya walinda amani yanaweza kujumuisha uhalifu wa kivita.

XS
SM
MD
LG