Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:25

Mkuu wa zamani wa IMF huenda akapunguziwa masharti ya dhamana.


Mkuu wa zamani wa IMF Dominique Strauss-Kahn na mawakili wake kwenye mahakama moja ya New York.
Mkuu wa zamani wa IMF Dominique Strauss-Kahn na mawakili wake kwenye mahakama moja ya New York.

Gazeti la New York Times limesema mlalamikaji ambaye ni mhamiaji kutoka Guinea amewadanganya mara kadhaa waendesha mashtaka

Mkuu wa zamani wa shirika la kimataifa la fedha duniani – IMF, Dominique Strauss Kahn atakwenda mahakamani Ijumaa huko New York kukutana na jaji wakati kesi dhdi yake ikisemekana iko kwenye mashaka makubwa kutokana na masuala ya kutokuaminika kwa mlalamikaji.

Mwanasiasa huyo mkongwe wa Ufaransa alikamatwa na kushtakiwa mwezi Mei kwa kumshambulia kingono mfanyakazi wa hoteli mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikwenda kusafisha chumba chake katika hoteli moja ya kifahari huko New York.

Gazeti la New York Times limesema mlalamikaji ambaye ni mhamiaji kutoka Guinea amewadanganya mara kadhaa waendesha mashtaka tangu alipotoa malalamiko yake ya kwanza. New York Times linaeleza kuwa yamegundulika mambo mengi ya kutia mashaka kuhusu historia ya mwanamke huyo, ikiwa ni pamoja na maombi yake ya hifadhi, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kushiriki katika harakati za kihalifu kama madawa ya kulevya na biashara haramu ya mzunguko wa fedha.

Strauss Khan amekana mashitaka hayo . Mawakili wake watamwomba jaji katika kesi ya Ijumaa kupunguza dhamana yake ya dola millioni 6 na kubadilisha masharti ya dhamana yake. Yupo chini ya ulinzi wa saa 24 kwenye nyumba ikiwa ni pamoja na kifaa cha kumlinda cha elektroniki, na ana itmu ya walinzi kwenye nyumba ya kukodisha anayoishi .

Masharti hayo yanamgaharimu dola 250,000 kwa mwezi.

XS
SM
MD
LG