Mkuu wa shirika la afya duniani (WHO) Jumatano ameshutumu hali katika eneo lenye mgogoro la Tigray nchini Ethiopia, na ameonya kwamba hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kuepuka kutokea mauaji ya kimbari.
Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaeleza wanahabari akiwa katika makao makuu ya WHO mjini Geneva kwamba dunia haiangalii inavyostahili hali hiyo na kwamba kuna kipindi kidogo kimebaki kuzuia mauaji ya kimbari katika eneo la Tigray.
Addis Ababa Jumanne ilisema imedhibiti miji mitatu katika mkoa huo wa kaskazini ambapo mapigano baina ya vikosi vinavyo unga mkono serekali na waasi wamekuwa wakipigana toka mwezi Agosti baada ya kuvunjika makubaliano ya kusitisha mapigano.
Wasiwasi wa kimataifa unaongezeka kwa wale waliopo katikati ya mapigano Tigrya ambapo vikosi vya Ethiopia na kutoka nchi jirani ya Eritrea kuanzisha mashambulizi yao.