Katibu Mkuu Antonio Guterres ameshutumu “mazingira hayo mabaya ya kuishi anayokabiliana nayo Rais Bazoum na familia yake kama ilivyoripotiwa,” kulingana na taarifa ya UN.
Kituo cha televisheni cha CNN kiliripoti Jumatano kuwa Bazoum amewekwa peke yake na kulazimishwa na waasi waliopindua serikali mwisho wa mwezi uliopita kula wali mkavu na pasta.
Katika mfululizo wa ujumbe wa maandishi Bazoum aliyompelekea rafiki yake, rais alisema alikuwa “amenyimwa mawasiliano yote ya watu tangu Ijumaa”, huku hakuna anayempelekea chakula au dawa, mtandao huo uliripoti.
Guterres “alirejea wasiwasi wake juu ya afya na usalama wa Rais na familia yake na mara nyingine tena ametaka aachiliwe mara moja, bila masharti yoyote na kurejeshwa katika nafasi yake ya urais,” msemaji wa Mkuu huyo wa UN aliandika katika taarifa yake.
Chanzo cha habari hii ni mashirika ya habari ya AFP na Reuters
Forum