Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:25

Mkuu wa sheria Eric Holder aelekea Ferguson, Missouri


Kikosi cha jeshi la ulinzi wa kitaifa Ferguson, Missouri, Aug. 18, 2014.
Kikosi cha jeshi la ulinzi wa kitaifa Ferguson, Missouri, Aug. 18, 2014.

Ghasia zaongezeka katika Ferguson, Missouri ambapo waandamanaji wanakabiliana vikali na polisi na jeshi la ulinzi wa kitaifa.

Rais wa Marekani Barack Obama anasema mkuu wa sheria nchini Marekani Eric Holder, atasafiri kuelekea Ferguson, katika jimbo la Missouri leo Jumatano, ili kupata tathmini mpya juu ya uchunguzi wa serikali kuu,kufuatia kuuawa kwa kijana mweusi wa Marekani, aliyepigwa risasi na polisi mzungu Agosti 9.

Kifo cha Michael Brown ambaye hakuwa na silaha kimeibua hisia kali miongoni mwa wamarekani weusi na kuzusha maandamano makali na makabiliano baina ya waandamanaji na polisi.Jumanne gavana wa jimbo hilo aliomba jeshi la ulinzi wa kitaifa kupelekwa huko Ferguson kusaidiana na maafisa wa polisi.

Marufuku ya kutotoka nje usiku iliondolewa Jumanne, lakini hali ilizidi kuwa tete na kubidi maafisa wa polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kukabiliana na waandamanaji.

Akizungumza jana jioni katika White House na waandishi habari, rais Obama alisema kwamba Bw. Holder atakutana na maafisa wa wizara ya sheria na wapelelezi wa idara makosa ya jinai F.B.I., kuhusiana na uchunguzi wa serikali kuu na uchunguzi huru wa kundi la haki za binadamu katika mauaji ya kijana huyo.

Holder pia atakutana na viongozi wa kijamii katika juhudi za kurejesha tena amani na utulivu katika kiunga hicho cha mji wa St.Louis.

Bw.Obama aliwaomba waandamanaji wajiepushe na ghasia, wasipore mali wala kushambulia maafisa wa polisi.

XS
SM
MD
LG