Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 21:13

Mkuu wa sera ya kigeni katika EU apendekeza vikwazo dhidi ya mawaziri wawili wa Israel


Josep Borrel, mkuu wa sera ya kigeni katika Umoja wa Ulaya
Josep Borrel, mkuu wa sera ya kigeni katika Umoja wa Ulaya

Mkuu wa sera ya kigeni katika Umoja wa Ulaya Josep Borrel Alhamisi alisema aliziomba nchi wanachama kutafakari uwezekano wa kuwawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israel kwa “ matamshi ya chuki” dhidi ya Wapalestina, matamshi ambayo amesema yanakiuka sheria ya kimataifa.

Hakutaja majina ya mawaziri hao. Lakini katika wiki za hivi karibuni alimkosoa hadharani waziri wa usalama Itamar Ben-Gvir na waziri wa fedha Bezalel Smotrich kwa kauli ambazo alizielezea kuwa “mbaya” na “uchochezi wa uhalifu wa kivita.”

Borrell alisema mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya walifanya majadiliano ya awali kuhusu pendekezo lake katika mkutano mjini Brussels Alhamisi.

Alisema hapakuwa muafaka ambao utahitajika ili kuweka wikwazo, lakini mjadala utaendelea.

“Mawaziri wataamua. Inawahusu kama kawaida. Lakini mchakato umeanzishwa,” aliwambia waandishi wa habari.

Alisema alipendekeza mawaziri hao wa Israel wachukuliwe vikwazo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa ujumla vinamaanisha kupiga marufuku kusafiri katika jumuia hiyo na kuzuiliwa kwa mali zinazomilikiwa ndani ya Umoja wa Ulaya.

Forum

XS
SM
MD
LG