Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 20:47

Mkuu wa Polisi Uganda awataka raia 'kuwakamata' polisi


Polisi wa Uganda wakifanya mazoezi.

Mkuu wa polisi nchini Uganda ameamrisha wananchi kuwakamata au kuwapiga mawe maafisa wa polisi wasiojitambulisha wanapokuja kuwakamata washukiwa hata kama wamebeba bunduki.

Raia wa Uganda wanadai kwamba wanashindwa kuwatambua wanaowateka nyara jamaa zao, kwani wana tabia sawa na za maafisa wa polisi, wanao wakamata raia bila ya kujitambulisha, wala kuvalia sare za kikazi.

"Afisa wa polisi anapewa mafunzo jinsi ya kumkamata mshukiwa. Anastahili kujitambulisha na kumweleza mshukiwa sababu za kumkamta kabla ya kumkata. Kama hafanyi hivyo, raia wawakamate au wawapige mawe," amesema Kamanda Okoth Ochola.

Karibu kila siku, matukio ya mtu kutekwa nyara, hasa wasichana na akina mama yamekuwa yakiripotiwa nchini Uganda.

Utekaji nyara pia umesambaa na kuwalenga watoto wadogo, chini ya miaka 5 licha ya maafisa wa polisi na jeshi kuingilia kati kukabiliana na watekaji nyara.

Mkuu wa polisi anahusisha utekaji nyara huo na makundi ya kigaidi, na amesema : "Baadhi ya washukiwa ambao tumewakamata wana uhusiano na makundi ya kigaidi lakini sitayataja kwa wakati huu kwa sababu bado tunafanya uchunguzi. Tutakapokamilisha uchunguzi wetu, tutawaeleza."

Visa vya utekaji nyara vimekuwa vikiendelea nchini Uganda kwa mda wa takriban mwaka mmjoa sasa. watekaji nyara hudai mamilioni ya pesa kama kikombozi, na hata baada ya kulipwa pesa wanazotaka, huwaua wale waliowateka nyara.

Wakati huohuo Polisi nchini Uganda pia wamewakamata wapiganaji wa Maimai 26 kutoka Jamhuri ya Kidemokraksia ya Congo (DRC), baada kikundi cha wapiganaji hao kuwateka nyara wavuvi 6 raia wa Uganda katika ziwa Edwward, magharibi mwa Uganda.

Wapiganaji wa mai mai wanataka sanduku kadhaa za risasi kama kikombozi. "Nasi, tumewakamata wapiganaji wao 26. Kwa hivyo tumewapa masharti kwamba waachilie raia wetu kwanza," amesema mkuu wa polisi wa Uganda Okoth Ochola.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire Washington DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG