Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:54

Rais wa kampuni ya Mitsubishi ajiuzulu


Mitsubishi President Tetsuro Aikawa listens to a reporter's question during a press conference in Tokyo, Wednesday, May 18, 2016.
Mitsubishi President Tetsuro Aikawa listens to a reporter's question during a press conference in Tokyo, Wednesday, May 18, 2016.

Mkuu wa kampuni ya utengenezaji magari ya Japan, Mitsubishi, Bwana Testuro Aikawa amejiuzulu baada ya kashfa kuibuka mwezi uliopita kuhusu kudanganya kiwango cha mafuta yanayotumika na magari hayo.

Aikawa alikuwa pamoja na mwenyekiti wa kampuni ya Mitsubishi, Osamu Masuko, mapema leo kutangaza kuachia ngazi kwake katika kampuni hiyo akiwajibika kutokana na kashfa hiyo. Hata hivyo amewaambia wanahabari kwamba anataka kuhakikisha uchunguzi unakamilika.

Mwezi uliopita, kampuni ya Mitsubishi ilikubali kwamba wafanyakazi wake waliongeza chumvi katika takwimu kwa kueleza kwamba magari yake yanatumia kiwango cha nafu cha mafuta kwa kila kilomita na hivyo kufanya aina kadhaa za magari yake kuonekana yana kiwango kidogo cha utumiaji wa mafuta kuliko kiwango halisi.

Mitsubishi ni kampuni nambari sita duniani katika utengenezaji magari imepoteza nusu ya thamani ya soko lake baada ya taarifa hizo kufichuka.

XS
SM
MD
LG