Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 15:59

Mkuu wa jeshi Sudan ataka mabadiliko kwenye utawala wake


Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, Jumapili ametoa mwito kwa wanajeshi kumaliza msaada kwa viongozi wa kimabavu.

Amesema hayo wakati mazungumzo yakianza ya mageuzi ya kijeshi, ikiwa ni sehemu ya kipindi cha mpito kilicho chukuwa muda mrefu kuelekea utawala wa kiraia.

Burhan aliingia madarakani katika mapinduzi ya 2021 ambayo yaliharibu kipindi kifupi cha mpito cha kidemokrasia kufuatia kuondolewa kwa aliyekuwa rais Omar al-Bashir 2019.

Marekebisho ya vikosi vya usalama ni hoja muhimu katika mvutano wa majadiliano juu ya mchakato wa kisiasa wa awamu mbili uliozinduliwa Desemba, ikifikiria kuondoa majenerali kwenye siasa mara tu serikali ya kiraia itakapowekwa.

Wakosoaji wana wasiwasi na mpango huo, uliokubaliwa na Burhan na vikundi mbalimbali pamoja na kambi kuu ya kiraia, wakisema haueleweki.

XS
SM
MD
LG