Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:50

Mkuu wa IAEA asema timu yake ipo njiani kutembelea kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia


Timu ya IAEA ikielekea Zaporizhzhya kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vienna,
Agosti 29, 2022. Picha na Dean Calma/IAEA/REUTERS.
Timu ya IAEA ikielekea Zaporizhzhya kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vienna, Agosti 29, 2022. Picha na Dean Calma/IAEA/REUTERS.

Mkuu wa idara ya Kimataifa ya Atomiki ya Umoja wa Mataifa – IAEA  anasema timu yake ipo njiani kutembelea kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kilichopo karibu na uwanja wa mapambano wa uvamiziwa Russia nchini Ukraine.

Mkurugenzi wa idara hiyo Rafael Mariano Grossi aliandika ujumbe wa Twitter kwamba anaongoza timu ambayo itakwenda katika kinu hicho wiki hii.

IAEA imesema kazi yake ikiwa huko itashughulikia kufanya tathimini ya uharibifu katika kinu, kuangalia usalama na mifumo ya ufanyaji kazi ya ulinzi, kukagua hali za wafanyakazi na kuangalia shughuli muhimu wa kiusalama, Russia imekuwa ikidhibiti eneo la kinu hicho toka mapema mwa uvamizi huo wa miezi sita, lakini kinu hicho kinaendeshwa na wahandisi wa Ukraine.

XS
SM
MD
LG