Watu wenye silaha kutoka Hamas waliwaua watu 1,200 na kuwachukua mateka 253 katika shambulizi la Oktoba 7 nchini Israel, kwa mujibu wa hesabu za Israel.
Shambulizi lilichochea majibu ya Israel huko Gaza ambayo inaendeshwa na Hamas, ambayo imesema azma yake ni kuwaokoa mateka waliobaki na kulitokomeza Hamas. Maafisa wa afya huko Gaza wanasema zaidi ya watu 30,000 wamethibitishwa kuuawa wakati wa vita hivyo.
Turk, ambaye aliwasilisha ripoti ya hali ya haki za binadamu huko Gaza na katika eneo linalokaliwa kimabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi, amesema ofisi yake imerekodi “matukio mengi ambayo yanapelekea uhalifu wa vita uliofanywa na majeshi ya Israel.”
Aliongezea kuwa pia kuna ishara kwamba majeshi ya Israel yamejihusisha katika kuwalenga “kiholela au bila mpangilio” ikiwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Turk amesema makundi yenye silaha ya Wapalestina yamefanya mshambulizi holela ya makombora katika eneo la kusini mwa Israel, na kuwashikilia mateka ambapo pia ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.
Israel inasema inafanya kila inaloweza kupunguza maumivu kwa raia.
Katika hotuba yake ambayo ilipongezwa na baadhi ya wale waliohudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa cha Haki za Binadamu mjini Geneva, Balozi wa Palestina Ibrahim Khraishi amesema “tunalaani kile ambacho kimetokea Oktoba 7 na tunafanya hivyo kwa uthabiti, lakini hakuna mtu amabye kwa kweli analaani kwamba wanawake, watoto na wazee wanauawa.
Forum