Jeshi la Israel, pia limeripoti mashambulizi mapya ya anga katika eneo la Khan Younis, kusini mwa Gaza, pamoja na operesheni za ardhini katika eneo hilo na kaskazini mwa Gaza.
Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, huko Gaza Jumatano imeripoti kuwa takriban watu zaidi ya 76 wameuawa katika kampeni za Israeli.
Takriban watu 29,954 wameuawa toka vita kuanza Oktoba mwaka jana, huku wengine 70,325 wakijeruhiwa. Wapatanishi wa Israel, Hamas na Qatar siku ya Jumanne wote walipuuza pendekezo la rais wa Marekani, Joe Biden, kwamba makubaliano mapya ya kusitisha mapigano na kuachiliwa mateka yanaweza kufikiwa.
Forum