Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:41

Viongozi wa Ulaya wajipanga kuendelea bila Uingereza


Angela Merkel
Angela Merkel

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanazingatia juu ya njia za kupanga mustakbali wao bila ya Uingereza, wakati wanakamilisha mkutano wao huko Brussels siku kadhaa baada ya Waingereza kupiga kura ya kuondoka kutoka kwenye Umoja huo.

Wametoa wito hii leo kwa Uingereza kuondoka haraka na kutotarajia kupata maslahi yeyote ya uanachama bila ya kukabiliwa na athari zake kwanza.

Mkutano huo unaonekana kuwa wa mwisho kwa waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, ambaye anajiuzulu baada ya serikali yake kushindwa kuwashawishi wapiga kura kuchagua kubaki ndani ya Umoja wa Ulaya.

David Cameron
David Cameron

Akizungumza baada ya mazungumzo alisema licha ya huzuni na kujuta, mkutano wa viongozi wa mataifa 28 ya Ulaya ulikuwa wenye mafanikio.

XS
SM
MD
LG