Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:48

Hali ya hewa kutawala mazungumzo ya Obama nchini Canada


Suala la mabadiliko ya hali ya hewa litapewa kipaumbele wakati wa mazungumzo ya Rais Barack Obama huko Canada leo Jumatano atakapo hudhuria mkutano wa viongozi wa Amerika ya Kaskazini, mjini Otawa.

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, na Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto, wataungana na Rais Obama katika kutangaza ushirikiano wa bara zima juu ya hali ya hewa unaolenga kuzalisha nusu ya umeme unaohitajika Amerika Kaskazini kutoka vyanzo visivyo zalisha gesi chafu za carbon ifikapo mwaka 2025.

Kwa hivi sasa ni karibu theluthi moja tu ya umeme wa bara hilo unatokana na vyanzo vya nishati safi kama vile upepo, jua, maji au nishati ya nyuklia.

Marekani na Canada tayari zimedhamiria kupunguza uzalishaji gesi ya methane kwa asili mia 40 hadi asilimia 45 chini ya viwango vya 2012.

XS
SM
MD
LG