Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:19

Mkutano wa SADC walenga swala la Zimbabwe


Viongozi kutoka Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC waanza mkutano nchini Namibia huku swala la Zimbabwe likipewa kipaumbele.

Viongozi kutoka jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika-SADC wameanza mkutano unaotarajiwa kulenga suala la Zimbabwe. Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma, ambaye anaongoza juhudi za upatanishi za SADC nchini Zimbabwe, anatarajiwa kutoa taarifa juu ya juhudi za kusukuma mbele mkataba wa kushirikiana madaraka nchini humo.

Sadc
Sadc

Katika taarifa ya jana, Afrika kusini ilisema Zimbabwe imepiga hatua kiuchumi. Pia ilisema kuna maendeleo kiasi katika mkataba wa kushirikiana madaraka, lakini majadiliano yanaendelea katika masuala kama uteuzi wa magavana wa majimbo.

XS
SM
MD
LG