Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 07:03

Pakistan na Afghanistan wamendelea kuamini ushirikiano wao


Pakistan na Afghanistan katika mazungumzo yao wamerudia tena kwamba “utawala wenye mafanikio kwenye mpaka wao wanaoshirikiana ni muhimu kwa juhudi zinazolenga kupambana na ugaidi, kuhamasisha amani na kuimarisha uhusiano wa pamoja."

Ujumbe wa wanachama sita wa Afghanistan unaoongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan, Hekmat Khalil Karzai, ulitembelea Islamabad leo Jumatatu kwa mazungumzo na wenzao wa Pakistan.

Mkutano ulifanyika kufuatia siku kadhaa za mapambano yaliyosababisha vifo kati ya nchi hizo mbili uliochochewa na ujenzi wa Pakistan wa geti jipya kwenye mji wenye harakati nyingi wa Torkham unaokatisha kuingina Afghanistan.

Mazungumzo kati ya wajumbe wa nchi hizi mbili yalifanyika katika mazingira rafiki yakiwa na matumaini ya pamoja ya kutatua masuala.

XS
SM
MD
LG