Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 10:48

Mkutano wa NATO Chicago


Zaidi ya nchi 50 zashiriki katika mkutano wa NATO Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen walifungua mkutano wa NATO mjini Chicago Jumapili wakisema kuwa viongozi wa dunia watapanga mikakati ya hali ya baadaye nchini Afghanistan katika kipindi cha muda wa siku mbili za mazungumzo.

Bwana Obama aliwaambia washiriki wa mkutano huo kwamba changamoto zingalipo na kwamba maisha ya watu wengi yatapotea. Lakini akaongeza kuwa kuna matumaini kwamba wamo katika njia sahihi na akisema mkutano huo wa NATO unaashiria dunia inaunga mkono mkakati ambao wameuweka.

Viongozi kutoka zaidi ya mataifa 50 walikaa kimya kwa muda wa dakika moja kutoa heshima kwa maelfu ya wanajeshi wa ushirika waliofariki au kujeruhiwa wakati wa vita nchini Afghanistan.

XS
SM
MD
LG