Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 22:56

Mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya hewa barani Afrika waanza mjini Nairobi


Mfanyakazi apita mbele ya bango la Mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika.
Mfanyakazi apita mbele ya bango la Mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika.

Mkutano wa kwanza wa bara la Afrika kuhusu mabadiliko ya hali ya unafunguliwa leo Jumatatu katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, ukiangazia bara ambalo litaathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa huku likichangia mabadiliko hayo, kwa kiasi kidogo zaidi.

Shirika la habari la AP linariporti kwamba uwekezaji mkubwa, katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika, ikiwa ni pamoja na utabiri wa kutegemewa, utakuwa moja ya malengo makuu.

Kiini cha kila suala kwenye ajenda, kutoka kwa nishati hadi kilimo, ni ukosefu wa ukusanyaji wa data ambao unasukuma maamuzi muhimu kama vile wakati wa kupanda - na wakati wa kutoroka maeneo ya makazi, kwa mujibu wa shirika hilo.

Bara la Afrika ni kubwa kuliko China, India na Marekani kwa pamoja, na ili hali ina vifaa vya rada 37 tu vya kufuatilia hali ya hewa, vyombo muhimu, pamoja na data za satelaiti, zinazofuatilia masuala ya hali ya hewa, kulingana na data ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani.

Kenya, mwenyeji wa mkutano huo wa hali ya hewa, ni mojawapo ya nchi chache barani Afrika zinazoelezwa kuwa na huduma ya hali ya hewa, ambayo imeimarishwa kwa kiasi fulani, nyingine zikiwa ni Afrika Kusini na Morocco. Taifa hilo la Afrika Mashariki limetenga takriban dola milioni 12 mwaka huu kwa huduma yake ya hali ya hewa, kulingana na wizara yake ya fedha.

Ikilinganishwa na kwingineko, ombi la bajeti ya Huduma ya Kitaifa ya Hali ya Hewa ya Marekani kwa mwaka wa fedha wa 2023 lilikuwa dola bilioni 1.3. Eneo kubwa la bara la Afrika lenye mataifa 54 halina huduma ya hali ya hewa ya kutegemewa.

Forum

XS
SM
MD
LG