Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:51

Mkutano wa kujadili kurejesha wakimbizi wa DRC makwao wavunjika Tanzania


Picha ya wakimbizi
Picha ya wakimbizi

Mkutano huo ulihusisha serikali ya tanzania, DRC na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi - UNHCR.


Mkutano wa kujadili zoezi la kuwarejesha makwao wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walioko kwenye kambi ya Nyarugusu iliyoko Kasulu mkoani Kigoma uliokuwa ukifanyika jijini Dar es salaam leo umevunjika kutokana na baadhi ya vipengele vilivyokuwa vimefikiwa katika vikao vilivyopita kutotekelezwa.

Mkutano huo ulihusisha serikali ya tanzania, DRC na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi - UNHCR.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuvunjika kwa mkutano huo waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa Tanzania, Shamsi Vuai Nahodha amesema serikali ya Tanzania imegomea kuendelea kwa mkutano huo kutokana na asilimia kubwa ya mambo waliyokuwa wameafikiana katika vikao vilivyopita kutotekelezwa hususan na upande wa serikali ya DRC.

Kwa mujibu wa waziri Nahodha, DRC imeomba miezi sita ya kufanya maandalizi yakuwapokea wakimbizi 62,000 walioko katika kambi hiyo ya Nyarugusu, ombi ambalo hata hivyo amesema Tanzania imelikubali lakini wakati huo huo ikiendelea kurejesha wakimbizi hao kwa makundi.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya kijamii na utu wa DRC aliyekuwa kiongozi wa ujumbe wa DRC kwenye mkutano huo, Kambere Kalumbi Ferdinand amesema wameomba kuongezewa muda kutokana na serikali yake kutokamilisha maandalizi ya kuwapokea hasa ikizingatiwa kwamba nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu.

XS
SM
MD
LG