Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:26

Obama kuongea na Shinzo Abe kwenye Mkutano wa G7 Japan


A security guard stands at the entrance of the international media center of the G7 Summit in Ise, Wednesday, May 25, 2016.
A security guard stands at the entrance of the international media center of the G7 Summit in Ise, Wednesday, May 25, 2016.

Maafisa wa Serikali za Japan na Marekani wanaeleza kwamba Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, atazungumzia swala la uhalifu uliotendwa na wafanyakazi katika kambi za kijeshi za Marekani wakati wa mkutano wake na Rais Obama alasiri ya leo, kabla ya mkutano wa mataifa saba yenye nguvu zaidi duniani G7.

Swala hilo limeongezwa kwa haraka katika ajenda ya mazungumzo kati ya viongozi hao wawili, kufuatia kukamatwa kwa mwanajeshi wa zamani wa Marekani siku ya Alhamisi iliyopita, kuhusiana na kupotea kwa mwanamke Mjapan mwenye umri wa miaka ishirini. Mwanamke huyo alipotea tarehe 28 mwezi uliopita na mwili wake ulipatikana wiki jana.

Kifo chake kimezua kumbukumbu za visa vya ubakaji wa wasichana wa shule uliofanyika katika kambi za kijeshi za Kimarekani kisiwani Okinawa mnamo mwaka wa 1995, jambo lililopelekea maandamano makubwa dhidi ya kambi za jeshi la Marekani.

XS
SM
MD
LG