Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:00

Mkutano wa G7: Wajadili hatua za kudhibiti moto msitu wa Amazon


Mkutano wa viongozi wa kundi la nchi saba tajiri zaidi dunaini - G7 umeanza Jumamosi kusini magharibi mwa Ufaransa.

Wachambuzi wanaeleza janga la moto unaoendelea kuwaka katika msitu wa Amazon, kutetereka kwa masoko ya hisa na tofauti kubwa zilizopo baina ya nchi hizo tajiri ni mambo yatayopewa kipaumbele katika mazungumzo yao.

Lakini pia waandamanaji tayari wamejipanga kuwapokea viongozi wa nchi hizo akiwemo Rais wa Marekani, Donald Trump na viongozi wenzake wa nchi za Magharibi wakati wakiwasili katika mji wa Biarritz.

Wakati huohuo polisi wamepelekwa kulinda doria ili kuzuia vurugu zozote zitakazo tokea wakati wa mkutano huo.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, mwenyeji wa mkutano wa G7 ametoa shinikizo kwa Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro kuruhusu jumuiya ya kimataifa kushiriki kusaidia kuzima moto unaoendelea kuangamiza msitu wa Amazon.

Rais Macron amesema Ufaransa itasitisha hatua za kufikia makubaliano ya kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Amerika Kusini.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG