Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 15:45

Mkutano wa G-20 wamalizika.


Viongozi wa nchini 20 zenye ustawi mkubwa wa kiviwanda , G20 waliokutana mjini Toronto, Canada, wametowa mwito kwa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani, kupunguza nakisi zao kwa nusu katika kipindi cha miaka 3.

Akiwahotubia viongozi wa G-20, waziri mkuu wa Canada, Stephen Harper, alisema uchumi wa dunia ulodhaifu, bado unahitaji juhudi za kifedha za kuufufua , lakini mataifa lazima yasonge mbele katika mpangilio maalum wa kupunguza nakisi.

Ili kuhimili ufufuzi, alisema mataifa lazima yatimize mipango ya kufufua uchumi walokubaliana nayo wakati wa mkutano wa awali huko Pittsburgh, akiongozea kuwa soko zisizothabiti, zinatuma ujumbe wa kuwepo kwa hatua zilopangwa na kuratibiwa.

Bw. Harper anasema mataifa ya G-20 yako katika hali tete inayowahitajia kufwatilia mipango iliopo, lakini pia kutuma ujumbe dhahiri kuwa pale mpango wa fedha za kufufua uchumi utakapomalizika, watatakiwa kuweza kusimamia mfumo yao ya kifedha.

“Lazima tukubali kuwa nakisi zitapunguzwa kwa nusu ifikapo 2013. Pia inafaa tukubali kuwa kiwango cha deni la taifa ikilinganishwa na pato la jumla la taifa lazima aidha yasawazishwe ifikapo mwaka 2016 au yawe katika hali ya kuendelea kupungua.”Amesema Harper.

Suala moja tete katika mkutano huo wa G-20, na pia katika mkutano wa G-8 hapo awali, ni juu ya mda wa kuhimili matumizi ya mpango wa kufufua uchumi ili kuhakikisha ukuzi. Rais Obama alieleza kuwa kupunguwa mapema kwa mpango wa kufufua uchumi huwenda kukasababisha kudumaa tena kwa uchumi wa dunia.

Katika mkutano wa G-20 uloanza hapo Jumamosi, waziri wa fedha wa marekani Tim Geithner, alibashiri kuwa viongozi wataafikiana juu ya uwamuzi muafaka baina ya mpango wa kufufua uchumi na kuchukuwa tahadhari , lakini akakariri tena kuwa wasiwasi wa Marekani juu ya kuurudi mpango wa kufufua uchumi haraka sana.

Chancellor wa Ujerumani Bi Angela Markel, alisema ukuwaji unaostahiki haubidi kuhitalafiana na hatua za upunguzaji matumizi zinazotekelezwa na baadhi ya nchi.

Bw. Obama alifanya mkutano na waandishi habari baada ya kumalizika kwa mkutano wa G-20, kabla kurejea Washington ambapo miongoni mwa mambo atakayoshugulikia ni, kusubiria hatua ya mwisho ya baraza la bunge la Marekani, juu ya marekebisho ya sheria za fedha.

XS
SM
MD
LG