Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 07:42

Trump, Xi kufanya mazungumzo Florida


Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson, kushoto, akiwa na Rais wa China Xi Jinping

Rais Donald Trump anakutana na Rais wa China Xi Jinping katika Jumba lake la Florida Alhamisi kwa mkutano wa siku mbili ambapo kiongozi wa Marekani anatarajia kuishinikiza Beijing kuchukua hatua zaidi kuidhibiti Korea Kusini kusitisha utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Bila ya kutoa maelezo zaidi, Trump ameonya wiki hii, “Iwapo China haitaweza kutatua mgogoro wa Korea Kaskazini, sisi tutachukua hatua.” Uongozi wake unakadiria kuweka vikwazo dhidi ya mabenki ya China na makampuni ambayo yanatoa fursa za mikopo kwa Pyongyang katika benki za kimataifa

China imekuwa ikiwapelekea Korea Kaskazini mahitaji yao yote ya mafuta. uingizaji chakula, bidhaa, na mali ghafi zinazotumika katika kujenga programu yao ya silaha.

Lakini China pia imechoshwa na matakwa ya kijeshi ya Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ambaye mpaka sasa hajatembelea Beijing wakati wote wa utawala wake katika kipindi cha miaka sita.

Katika mlolongo wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini havijaweza kuizuia kufanya majaribio ya mfululizo wa makombora, na kuwa jaribio la karibuni kabisa lilifanyika wiki hii.

Trump na Xi, ni viongozi wa mataifa makuu mawili ya uchumi mkubwa ulimwenguni, wanakutana kwa mara ya kwanza na wamepangiwa kufanya mazungumzo Ijumaa baada ya chakula cha usiku Alhamisi wakiwa na wake zao katika makazi ya Trump ya kifahari ya Mar-a-Lago.

XS
SM
MD
LG