Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:18

Trump atabiri mazungumzo na Xi yatakuwa ‘Mazuri,’ ‘Magumu’


Rais Donald Trump- Rais Xi Jinping

Rais Donald Trump anatarajiwa kumpokea Rais wa China Xi Jinping kuanzia Alhamisi katika Jumba lake la Mara-Lago lilioko ufukweni katika eneo la Kusini ya Marekani.

Lakini inawezekana hali halisi isiwe ya uchangamfu kama ilivyo hali ya hewa ya Florida.
Trump ametuma kupitia Twitter utabiri wake kuhusu mkutano wake wa kwanza na Rais wa China, akisema utakuwa na mazungumzo “magumu sana,” kwani Marekani “haiwezi kukubali kubakia kuwa na upungufu wa kibiashara na uhaba wa ajira.”

Katika mkutano wake ikulu ya White House wiki iliopita, Trump aliwaambia wenye viwanda vilivyoko Marekani watakuja “kushangaa” watapomuona akiwa na Xi.

“Natarajia kwa hamu kubwa kukutana naye na ujumbe wake. Na tutaona kile kitakachotokea,”amesema Trump. Kiongozi huyo wa China sio rahisi kuja mikono mitupu.

“Nimatarajio yangu kuwa Wachina watamtuma Xi hapa akiwa na kitita cha zawadi kubwa nzuri na za ukarimu, katika masuala ya uwekezaji wa miundo mbinu ndani ya Marekani, na kumsaidia Rais Trump kuleta ajira ambazo alikuwa amewaahidi wapiga kura,” Mtafiti wa ngazi ya juu wa Stimson Center Yun Sun ameiambia VOA.

“Jambo la kijinga linaweza kutokea…’

Baadhi ya wanaofuatilia China wametahadharisha kuwa sio kila kitu kitaenda vile kilivyopangwa, kwani jambo hili ni mapema sana kwa uongozi wa Trump kwani mengi bado hayajaorodheshwa.

“Kitu cha kijinga kinaweza kutokea bila ya kutarajia, bila shaka. Unajua ujumbe mmoja wa Tweet unaweza kubadilisha muelekeo wa mkutano kwa kiwango fulani,” amesema naibu mkurugenzi wa tafiti za China (CSIS), Scott Kennedy.

“Lakini ninategemea kutakuwa na lawama bila ya kuwa hasa na mazungumzo mengi, na baadae Wachina wataondoka wakiwa na wasiwasi.”

XS
SM
MD
LG