Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 05:49

Mkutano wa China na Afrika wamalizika Johanesburg


Rais wa China Xi Jimping akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano

Viongozi hao walikutana kwa kile ambacho rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anasema ni mazungumzo ya kihistoria, yenye lengo za kuimarisha ushirikiano baina ya bara hilo na msharika wake mkubwa wa kibiashara.

Nchi 50 za Africa na China zimekamilisha mkutano Jumamosi mjini Johanesburg , Afrika Kuisini na kuahidi kuchochea kupata suluhu ya amani na usalama katika bara la Afrika.

Viongozi hao walikutana kwa kile ambacho rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anasema ni mazungumzo ya kihistoria, yenye lengo za kuimarisha ushirikiano baina ya bara hilo na msharika wake mkubwa wa kibiashara.

Mkutano wa viongozi wa China na Afrika
Mkutano wa viongozi wa China na Afrika

Katika makubaliano yaliyofikiwa mjini Johanesburg viongozi hao wameahidi wataunga mkono suala la usalama na kuimarisha amani kwa njia ya mjadala, na mashauriano ambapo China pia iliingunga mkono Afrika dhidi ya kutafuta suluhu hizo.

Mkutano huo wa ushirikiano wa China na Afrika umefanyika kwa mara ya kwanza katika nchi ya bara la Afrika.

China imetoa dola bilioni 60 za kimarekani kulenga maeneo kumi ikiwemo viwanda, miundombinu, huduma za kifedha, kutokomeza umasikini ,usalama, na amani.

Katika fedha hizo dola milioni 60 zitatumika kuimarisha jeshi la pamoja la dharura la umoja wa Afrika ambalo litaweza kuwajibika mara moja wakati kunapotokea mizozo kote kwenye bara la afrika.

XS
SM
MD
LG