Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 21:02

Mkutano mkuu wa mazingira COP26 waanza mjini Glasgow, Scotland


Rais wa COP26, Alok Sharma, wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira mjini Glasgow, Scotland.
Rais wa COP26, Alok Sharma, wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira mjini Glasgow, Scotland.

Mkutano mkuu wa mazingira wa Umoja wa mataifa, COP26, ulifunguliwa rasmi Jumapili mjini Glogow, Scotland, ambapo wawakilishi kutoka takriban nchi 200 wanatarajiwa kuhudhuria.

Ni mkutano wa wiki mbili za mazungumzo ya kina ya kidiplomasia, yakiangazia namna ya kukabiliana na changamoto ya pamoja ya ongezeko la joto duniani.

Matukio makuu yanayopewa kipaumbale ni athari za mabadiliko ya hali ya hewa, zikiwa ni pamoja na ongezeko la joto duniani, mafuriko na kuongezeka kwa mioto ya misituni.

Rekodi za umoja wa mataifa zimeonyesha kuwa muongo uliopita ulikuwa wa joto jingi Zaidi, hali ambayo inapelekea wataalam kuonya kuhusu umuhimu mkubwa wa mikakati mahsusi ya kukabiliana na mabadiliko hayo.

Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ya kimataifa, na ulicheleweshwa kwa mwaka mmoja kwa sababu ya janga hilo.

Katika hafla ya ufunguzi huo Jumapili, maafisa wa umoja wa mataifa walianza kwa kuelezea masuala muhimu ya kujadiliwa kabla ya duru itakayowakutanisha viongozi wa juu kutoka nchi mbalimbali za dunia.

Mwenyekiti anayeondoka Carolina Schmidt aliyafungua mazungumzo ya Glosgow, kwa kuwataka waliohudhuria kukaa kimya kwa dakika moja, kwa heshima ya waliopoteza maisha kutokana na janga la Covid-19, tangu kufanyika kwa mkutano wa mwisho wa hali ya hewa, mnamo mwaka wa 2019.

Viongozi wa nchi mbalimbali wanatarajiwa kukusanyika Jumatatu mjini Glasgow, kuhudhuria mkutano huo, ambao umetanguliwa na ule wa viongozi wan chi zenye uchumi mkubwa Zaidi duniani G20, uliofanyika mjini Roma, Italia.

XS
SM
MD
LG