Wawakilishi wa shirika la fedha la kimataifa IMF, Benki ya Dunia na wizara ya fedha ya China, wameshiriki katika mkutano huo uliojadili namna ya kuweka mipango mipya ya kulipa madeni kwa nchi zenye kipato cha chini, asilimia 60 ambazo IMF inasema zinakabiliwa na hali ngumu ya kulipa madeni au zinakaribia kushindwa kulipa madeni yao.
Wataalam wa uchumi na watafiti kama Hary Verhoeven, ameiambia sauti ya Amerika kwamba uhusiano kati ya IMF na China, ambao ni wakopeshaji wakubwa kute duniani, haujakuwa mzuri.
Nchi za Afrika zilitarajia mkutano huo kuandika upya namna ya kulipa madeni yake au kusamehewa madeni hayo.
Zambia ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kushindwa kulipa madeni yake mwaka 2020 na kupelekea wakopeshaji wake kukubali kuisamehe madeni inayodaiwa.