Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:01

Mkutano wa Marekani na viongozi wa Afrika waanza leo


Waziri mkuu wa Guinea Mohammed Said Fofana akiwasili uwanja wa ndege wa Andrews Air force Base, Agosti 2, 2014
Waziri mkuu wa Guinea Mohammed Said Fofana akiwasili uwanja wa ndege wa Andrews Air force Base, Agosti 2, 2014

Viongozi 50 kutoka bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria mkutano huo wa siku tatu mjini Washington DC, ambapo Marekani imetangaza kuwa itatoa karibu dola bilioni moja kusaida miradi mbalimbali barani humo.

Marekani inatarajiwa kutangaza mabilioni ya dola za msaada kwa bara la Afrika katika mkutano wake na viongozi wa bara hilo unaoanza leo Jumatatu.

Viongozi 50 kutoka bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria mkutano huo wa siku tatu mjini Washington DC, ambapo Marekani imetangaza kuwa itatoa karibu dola bilioni moja kusaida miradi ya kibiashara, fedha zaidi kwa walinda amani na mabilioni ya dola kwa miradi ya chakula na nishati kwa bara hilo.

China, Ulaya na Japan zote zimejaribu kutoa misaada kama hiyo ili kuinua uwekezaji Afrika lakini White house inapinga kwamba mkutano huu ni hatua ya kukabiliana na ongezeko la uwekezaji wa China barani humo.

XS
SM
MD
LG