Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:25

Mkurugenzi wa WHO anaendelea na wadhifa wake kwa miaka mitano mingine


Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus

Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesusya alikuwa mgombea pekee aliyependekezwa na nchi 28 wanadiplomasia wa magharibi walisema Ijumaa. Mataifa hayo yanajumuisha wanachama wa Umoja wa ulaya, na nchi tatu za Afrika yaliliambia shirika la habari la Reuters

Tedros Adhanom Ghebreyesus anatarajiwa hivi sasa kuhudumu kwa muhula wa pili wa miaka mitano kama mkuu wa shirika la afya Duniani (WHO) baada ya kuwa mgombea pekee aliyependekezwa na nchi 28, wanadiplomasia wa magharibi walisema Ijumaa.

Wanadiplomasia hao walikuwa wakinukuu barua iliyotumwa na WHO kwa nchi wanachama wake 194 ikiziarifu kuhusu uteuzi wa siri uliomo kwenye bahasha zilizofungwa zilizowasilishwa mwishoni mwa Septemba.

Mataifa hayo 28 yanajumuisha wanachama wa Umoja wa ulaya, na nchi tatu za Afrika yaliliambia shirika la habari la Reuters. Hapo awali msemaji wa WHO, Margaret Harris alipoulizwa katika mkutano wa Geneva kuhusu uteuzi huo alisema kuwa shirika la Umoja wa Mataifa litatoa taarifa baadae leo Ijumaa.

XS
SM
MD
LG