Ushaidi wa Shou Zi Chew Alhamisi ulikuja wakati muhimu kwa kampuni hiyo ambayo ina watumiaji milioni 150 wamarekani lakini iko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa maafisa wa Marekani wanaohusika na usalama wa data na usalama wa watumiaji.
TikTok na kampuni yake mama ya ByteDance wameingizwa katika vita vya siasa za kimataifa kati ya Beijing na Washington juu ya biashara na teknolojia. Chew mzaliwa wa Singapore mwenye umri wa miaka 40 alijitokeza hadharani katika hatua nadra kukabiliana na madai ambayo TikTok imekuwa ikikabiliwa nayo.
"Tunaamini kinachohitajika ni sheria zilizo wazi ambazo zinatumika kwa jumla kwa kampuni zote za teknolojia," Chew alisema.
Iwapo marufuku hiyo itateklezwa, itakuwa ni mara ya kwanza kwa hatua kama hiyo kuchukuliwa na serikali ya Marekani kwa kampuni kama hiyo.