Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:36

Mkenya aweka rekodi mpya ya marathon duniani


Patrick Makau wa Kenya askimaliza Berlin Marathon katika rekodi mpya ya dunia saa 2, dakika 3, sekunde 38.
Patrick Makau wa Kenya askimaliza Berlin Marathon katika rekodi mpya ya dunia saa 2, dakika 3, sekunde 38.

Wakenya wengine wawili Chemlany na Kimaiyo wamaliza katika nafasi za pili na tatu

Mwanariadha wa Kenya Patrick Makau ameweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za marathon mjini Berlin Jumapili baada ya kumaliza mbio hizo katika muda wa saa mbili, dakika tatu na sekund 38.

Naye mwanadada wa Kenya Florence Kiplagat alishinda upande wa wanawake katika muda wa saa mbili, dakika 19 na sekunde 43.

Makau aliongoza ushindi wa Kenya katika mbio hizo huku Stephen Kwelio Chemlany akichukua nafasi ya pili na Edwin Kimaiyo akishika nafasi ya tatu.

Haile Gebrselassie wa Ethiopia aliyekuwa akishikilia rekodi ya dunia alishindwa kumaliza mbio hizo na akajitoa katika kilomita ya 35 kama alivyofanya katika mbio za New York Novemba mwaka jana. Gebrselassie alikuwa anajaribu kupata muda utakaomwezesha kushiriki katika mashindano ya Olimpiki mwakani mjini London.

Makau, mwenye umri wa miaka 26, alikuwa anatetea ubingwa wake baada ya kushinda mbio hizo za Berlin mwaka jana

XS
SM
MD
LG