Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 29, 2020 Local time: 07:56

Mke wa rais wa zamani wa Marekani afariki dunia


Mke wa rais wa 41 wa Marekani, mama Barbara Bush.

Mke wa rais wa 41 wa Marekani, George H W Bush, mama Barbara Bush amefariki dunia.

Mama Bush ambaye pia ni mama wa rais wa zamani wa Marekani, George W Bush,amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na ofisi ya rais George H W Bush na ilieleza kifo chake kimetokana na matatizo ya kiafya.

Mara kadhaa mama Bush alilazwa hospitalini mara kadhaa, ambapo siku ya Jumapili aliamua abakie nyumbani akiwa na familia yake.

Januari mwaka 2017, yeye na mumewe rais mstaafu Bush walilazwa kwa wakati mmoja. Yeye alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya koo, huku mumewe akitibiwa kwa ugonjwa wa nyumonia.

Mama Bush ni mmoja kati wanawake wawili tu nchini Marekani, kuwahi kuwa mke wa rais na mama wa rais. Abigail Adams alikuwa mke wa John Adams, na mama wa rais John Quincy Adams, rais wa sita wa Marekani.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG