Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 13:00

Mke wa Mugabe akataliwa visa ya Uswisi


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe .
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe .

Mke wa rais wa Zimbabwe na maafisa wake watano wamekataliwa viza ya kwenda Uswisi lakini ubalozi wa nchi hiyo huko Zimbabwe wakataa kutoa maelezo yeyote .

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefuta mpango wa kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa huko Switzerland wiki hii baada ya mkewe na maafisa wake watano kukataliwa Visa.

Vyombo vya habari vya serikali leo vilimnukuu afisa mmoja wa masuala ya nje ambaye hakutaka jina lake litajwe ambaye aliita uamuzi wa Uswisi wa visa ni wa “kujutiwa sana.” Afisa huyo alishutumu Uswisi kwa kukiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa na haki ya Zimbabwe ya kuchagua ujumbe wake wenyewe.

Ubalozi wa Uswisi nchini Zimbabwe umekataa kuzungumzia lolote kuhusu hilo. Umoja wa Ulaya na Marekani umeweka vikwazo vya usafiri na masuala ya kifedha kwa Bwana Mugabe na darzeni za wafanyakazi wake ambao wanawatuhumu kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa kisiasa.

Bwana Mugabe na ujumbe wake walikuwa wamepanga kwenda Geneva wiki hii kwa ajili ya mkutano wa masuala ya teknolojia ya mawasiliano.


XS
SM
MD
LG