Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 15, 2022 Local time: 20:02

Mmarekani mwengine ashikiliwa Korea Kaskazini


Chuo Kikuu cha PUST Korea Kaskazini

Mke wa raia wa Marekani aliyekamatwa na serikali ya Korea Kaskazini wakati wa wikiendi anaomba mumewe aachiliwe mara moja.

“Natumai kila mmoja ataungana na mimi katika kulitafutia ufumbuzi suala hili kwa haraka,” amesema Kim Mi Ok, mke wa mtafiti wa kilimo Kim Hak-song, ambaye alitiwa nguvuni siku Jumamosi kwa kushukiwa “ni tishio” dhidi ya Serikali ya Korea Kaskazini.

Shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini KCNA limeripoti Jumapili kwamba “chombo husika kinakamilisha uchunguzi wa kina” juu ya makosa ya jinai ya Kim, lakini halikutoa maelezo zaidi kuhusu kuzuilwa kwake.

Kukamatwa kwa Kim, ambaye alikuwa anafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Science na teknolojia cha Pyongyang (PUST), imefanya idadi ya Wamarekani wanaoishikiliwa na Korea Kaskazini kufikia wanne wakati kuna mvutano unaoongezeka kuhusu programu ya kutengeneza silaha ya nyuklia nchini humo.

PUST, ambayo imewaajiri idadi kubwa ya wafanyakazi wa kigeni, imetoa tamko ikisema, “Tunafahamu kwamba kuzuiliwa huku kunahusiana na masuala ya kiuchunguzi ambayo hayana mahusiano yoyote na shughuli za PUST.

Akizungumza na VOA Jumapili, Kim Mi Ok amesema mumewe alikamatwa alipokuwa akijaribu kurudi nyumbani kwake huko Dandong, China. Amesema PUST imemwambia kwa njia ya simu kwamba Kim alikuwa tayari ameshapanda train huko Pyongyang. Lakini, hakuweza kufika mwisho wa safari yake.

“Nilikwenda kumpokea katika kituo cha Dandong, na nikasubiri mpaka mtu wa mwisho aliposhuka kutoka kwenye treni, lakini hakuweza kuonekana,” amesema mke wa Kim, ambaye ni mmoja kati Wakorea milioni 2 waliozaliwa China.

XS
SM
MD
LG