Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 21:24

Mkataba wa Camp David unaelezwa kuwa unaweza kusababisha Beijing kufanya uchokozi zaidi


Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) na Rais Xi Jinping wa China.
Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) na Rais Xi Jinping wa China.

Mkataba wa Ulinzi wa pande tatu wa Camp David kati ya Marekani, Japan na Korea Kusini kuna uwezekano ukasababisha Beijing kufanya uchokozi zaidi katika bahari ya South China Sea, wachambuzi wanasema.

Mkutano huo wa pande tatu, wa viongozi wanaokutana wao wenyewe wa kwanza kutoka nchi hizo tatu, ulikubaliana kuchukua hatua za kiusalama zenye lengo la moja kwa moja katika kile washiriki hao walichokieleza katika taarifa yao ya pamoja kuwa “tabia ya uchokozi na hatari” ya China, hususan katika eneo la bahari ya South China Sea.

Mkataba huo unataka washirika hao watatu kuweka nia ya dhati kushauriana pamoja katika kuratibu majibu yao kukabiliana na vitisho vya kikanda.

Pia inawataka wapanue mazoezi ya pamoja ya kijeshi na kufanya mazungumzo kila mwaka. Katika taarifa hiyo, nchi hizo tatu zimeitaja China kwa “tabia yake ya uchokozi na hatarishi ikishikilia madai yasiyo halali ya eneo la baharini” katika kile kilichojitokeza kama kukemea uchokozi wa China katika bahari ya South China Sea.

Clint Work, mtafiti na mkurugenzi wa masuala ya mafunzo katika taasisi ya Korea Economic Institute of America, aliiambia Sauti ya Amerika katika mahojiano kuwa kutajwa moja kwa moja kwa tabia ya China katika bahari ya South China Sea na madai yake haijawahi kuwepo katika taarifa zilizopita zilizotolewa na Marekani na Korea Kusini.

“Kutaja kinagaubaga tabia zote hizi za China na madai yake ni hatua mpya. Na kuwekwa matamko haya katika nyaraka ya pande tatu ni jambo la kipekee,” alisema.

China's protest

Beijing ilieleza kukerwa na mkutano huu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Wang Wenbin aliuita mkutano huo “ni kitendo kamili cha kuingilia kati masuala ya ndani ya China, na jaribio la makusudi kupandikiza chuki” kati ya Beijing na majirani zake.

Msemaji huyo pia alitupilia mbali ukosoaji wa vitendo vya Beijing inavyofanya katika bahari ya South China Sea.

Forum

XS
SM
MD
LG