Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 09:37

Mkakati wa usalama wazinduliwa Kenya


Uhuru Kenyata, kiongozi wa muungano wao wa Jubilee

Kenya imeandaa mkakati wa usalama ambao utatumika wakati wa kampeni na uchaguzi.

Mkakati huo utajumuisha maafisa 180,000 watakaopata mafunzo kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu Agosti 8.

Mpango huo utawawezesha Wakenya kushiriki katika uchaguzi katika njia inayodumisha umoja wa nchi na maafisa watakuwepo kulinda usalama kuzuia vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani au visa vyovyote vya kuzua rabsha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkakati huo Mwenyekiti wa Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa Francis Ole Kaparo amewataka Wakenya kushiriki zoezi la uchaguzi kwa amani.

Aliwataka washikadau wote kuhakikisha kila kitu kiko shwari kudhibiti rabsha za aina yoyote katika uchaguzi mkuu akirudia kutahadharisha yale yalioshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/8 ambapo wakenya takriban 1000 walipoteza maisha yao na wengine 600,000 kuachwa bila makazi.

Amesema kuwa mpango huu utakuwa wa kuongeza ushirikiano kati ya polisi, umma, IEBC na tume nyingine huru.

Mkakati huu pia utatumika kwa ajili ya kukuza na kuhakikisha usalama wakati wa kipindi cha kampeni kupitia mbinu bora katika usimamizi wa mazungumzo ya umma kwa njia iliyo na utaratibu.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati, Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet, Mwenyekiti wa Mamlaka Huru ya Kuratibu utendakazi wa Idara ya Polisi (IPOA) Macharia Njeru.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG