Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:44

Rais wa Nigeria azindua mpango kusafisha Niger Delta


Rais Muhammad Buhari wa Nigeria anazindua mkakati wa kusafisha eneo lenye utata la uzalishaji wa mafuta la Ogoni katika jimbo la Rivers wakati wa ziara yake ya pili katika eneo la Niger Delta toka alipoingia madarakani mwaka mmoja uliopita.

Uzinduzi huo ni utekelezwaji wa ripoti ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa mazingira (UNEP), na hatua hiyo inaashiria ahadi yake katika eneo hilo lenye utajiri wa mafuta licha ya kuendele kwa ghasia kutoka kwa wanamgambo wanaopinga sera za Rais Buhari.

Vitendo vya wanamgambo hao wanaojiita 'Niger Delta Avengers' vimeshusha uzalishaji wa mafuta wa Nigeria kwa kipindi cha miaka 20. Licha ya kutofautiana kisiasa Gavana wa eneo hilo Nyesom Wike hapo jana alisifia juhudi za Rais katika kutekeleza ripoti jambo ambalo limesubiriwa kwa kipindi kirefu.

XS
SM
MD
LG