Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 26, 2022 Local time: 11:44

Mji wa kale wagunduliwa Misri


Zahi Hawass, Mkuu wa idara ya mambo ya kale Misri akionyesha moja ya ugunduzi wake Mei, 2010.

Maafisa wa Misri wanasema wataalam wa mambo ya kale wamegundua makazi ya watu yaliyokaliwa kiasi cha miaka 3,500 iliyopita.

Maafisa wa Misri wanasema wataalam wa mambo ya kale wamegundua eneo lililokuwa mji wa watu kiasi cha miaka 3,500 katika njia iliyokuwa ikitumiwa katika biashara ya eneo la Sahara.

Timu wa wataalam kutoka Misri na chuo kikuu cha Yale nchini Marekani walichimbua mji huo wa zamani kusini mwa jangwa la Misri linalojulikana kama El-Kharga magharibi ya nchi hiyo.

Mkuu wa mambo ya kale wa Misri, Zahi Hawass, anasema mji huo ulikuwa na ukubwa wa kilomita moja urefu na mita 250 upana, na unaelekea ulikuwa kituo kikuu cha shughuli za utawala kwa wanajeshi waliokuwa safarini wakati huo.

Mji huo wa kale uko katika eneo lililokuwa njia kuu ya misafara ya biashara ambayo ilikuwa inaunganisha bonde la Nile na vituo vingine na kuelekea hadi eneo la magharibi la Sudan ya sasa.

XS
SM
MD
LG