Wanajeshi wa vikosi maalumu vya Iraq wameliteka tena jengo la halmashauri ya mji wa Fallujah kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State leo Ijumaa baada ya mapambano ya takriban mwezi mmoja kuufikia mji.
Mji huo uliowahi kuwa ngome ya wanamgambo wa IS, vikosi vya Iraq vinavyoungwa mkono na mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani vimeweza kuwasukuma IS kati kati ya mji na kuweka alama ya ushindi kwa vikosi vya ushirika, mkuu wa jeshi la polisi nchini Iraq, alisema.
IS iliuteka mji wa Fallujah mwaka 2014, lakini baada ya mapambano makali zaidi ya mwezi uliopita, vikosi vya Iraq vimeweza kuuteka tena takribani nusu ya mji.
Katika mapambano haya mapya, vikosi viliingia kwenye mji takriban saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za huko na walikutana na udhibiti mdogo sana kutoka kwa wanamgambo wa IS.