Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 02, 2024 Local time: 08:42

Mji wa China wa Shangai waripoti vifo 39 kutokana na Covid 19


Uzio wa kijani umefunga milango ya maduka na nyumba kando ya barabara, huku kukiwa mlipuko wa ugonjwa wa corona katika mji wa Shangai, April 24, 2022. Picha ya Reuters.
Uzio wa kijani umefunga milango ya maduka na nyumba kando ya barabara, huku kukiwa mlipuko wa ugonjwa wa corona katika mji wa Shangai, April 24, 2022. Picha ya Reuters.

Mji wa China wa Shangai Jumapili umeripoti vifo 39 kutokana na Covid 19, ikiwa idadi kubwa ya vifo licha ya kuweka masharti makali ya kupambana na ugonjwa huo kwa wiki kadhaa, huku mji mkuu Beijing ukionya juu ya hali mbaya na kuongezeka kwa maambukizi.

Taifa hilo la pili lenye uchumi mkubwa duniani limekuwa likisumbuka kudhibiti mlipuko wake mbaya katika miaka miwili, huku likiweka masharti makali kwa kufunga shughuli zote na kufanya upimaji wa watu wengi kwa kushikilia sera kali ya kutopatikana hata kisa kimoja cha maambukizi ya Covid, ikiathiri sana biashara na ari ya umma.

Mji ambao ni kitovu cha biashara wa Shangai umefungwa kabisa tangu mwanzoni mwa mwezi huu, na hivo kusababisha tatizo la usambazaji wa bidhaa, huku wakazi wengi wakizuiliwa majumbani mwao kwa muda mrefu zaidi kwa sababu umekuwa kitovu cha mlipuko wa Covid 19.

XS
SM
MD
LG