Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 18:54

Vision 2020 kuboresha afya ya macho katika nchi maskini


J. Kevin White alitengeneza kifaa cha gharama nafuu ambacho watu wanaweza kukitumia kuchunguza tatizo la macho.
J. Kevin White alitengeneza kifaa cha gharama nafuu ambacho watu wanaweza kukitumia kuchunguza tatizo la macho.

Mara baada ya mwanamke mmoja kufanyiwa vipimo aliweza kutambua herufi umbali wa mita sita kutoka alipokuwa amesimama.

Jaribu kufikiria umekaa darasani na huwezi kuona picha ambayo mwalimu anakuonyesha. Fikiria unaendesha gari, bila ya kutambua kuwa huoni vizuri, na kwa hiyo udereva wako una hatarisha maisha yako na ya watu wengine. Lakini hivi leo hali hii kwa mamilioni ya watu ni ya kawaida.

Hi ni kwa sababu hakuna wataalamu wa afya ya macho, wanaojulikana kama “optometrists” kuweza kugundua tatizo la macho na kulitibu katika nchi nyingi za kipato cha chini duniani. Katika baadhi ya nchi zinazoendelea kuna mtaalamu mmoja kwa kila watu milioni nane.

Makadirio hayo yanatoka kwa J. Kevin White, ambaye alianzisha kikundi cha Global Vision 2020 ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji.

Global Vision 2020 ni kikundi cha hiari kilichoko Maryland nchini Marekani ambacho kinajiandaa kuwapima watu macho na kutoa miwani ya bei nafuu kwa wananchi katiak nchi zinazoendelea.

Bila shaka miwani yanawawezesha watu wenye tatizo la macho kuona vizuri, amesema White.

“Hata kama unajua kwamba unahitaji miwani, jambo ambalo wengi hawajui, bado nafasi ya kupata msaada ni finyu sana na gharama bado ziko juu," alisema.

Mtu anatarajiwa kulipa dola za Marekani 100 kwa kufanya vipimo vya macho na kupatiwa miwani. Hii gharama kwa wengi katika nchi nyingi zinazoendelea iko juu, sehemu ambazo watu kipato chao ni dola mbili au chini ya dola mbili kwa siku, alisema.

Lakini White ametengeneza kifaa cha gharama nafuu ambacho waalimu, wauguzii, na pengine kila mtu anaweza kufundishwa namna ya kukitumia na kugundua kwa haraka iwapo mtoto au mtu mzima anahitaji miwani.

White ameuonyesha mfumo huo katika mgahawa karibu na ofisi za Global Vision zilizoko Easton, Maryland. Katika muda wa chini ya dakika tano, alimpima nguvu ya macho mwanamke mmoja ambaye hakuweza kuona vitu vizuri kutoka mbali. Baadae alichagua lensi inayomfaa na kuziweka katika fremu ya miwani.

XS
SM
MD
LG