Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 07:20

Marekani kuangalia zaidi mitandao ya kijamii


Serikali ya Marekani imeongeza ufuatiliaji wake wa matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuweza kufahamu kuhusu nani anaweza kuwa tishio kwa usalama nchini.

Mfano wa hivi karibuni ni pendekezo kutoka Idara ya Uhamiaji kuwaomba wasafiri wa nje kutoa taarifa kuhusu akaunti zao kwenye huduma za mtandao wa kijamii kama vile Facebook na Twitter.

Maswali hayo yatajitokeza kama ya hiari kwenye fomu ambazo watu wanatakiwa kujaza wanapowasili au kuwasilisha taarifa awali kwenye mtandao kama vile jina, anuani, simu na jina la nchi walizotembelea tangu mwaka 2011.

Itatumika kwa wasafiri pekee kutoka nchi 38 ambao wanaruhusiwa kuingia Marekani bila visa.

XS
SM
MD
LG