Msako wa siku nzima katika vyumba vya kuhifadhi maiti unaendelea jijini Kampala Uganda kuutafuta mwili wa aliyekuwa mlinzi mkuu wa mgombezi wa urais Amama Mbabazi, Christopher Aine.
Msako umechochewa na gazeti moja jijini Kampala kuchapisha picha inayodaiwa kuwa ya mwili wa Aine ukivalishwa nguo katika chumba cha kuhifadhi maiti. Familia ya Aine imeshurutisha maafisa polisi kufanya msako huo.