Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:09

El Sissi akana kuipatia Saudia Arabia visiwa vyake


Rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi akiwa na mfalme wa Saudi Arabia, Salman Cairo, April 9, 2016.
Rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi akiwa na mfalme wa Saudi Arabia, Salman Cairo, April 9, 2016.

El-Sisi alilihutubia taifa kupitia televisheni kuwahakikishia Wamisri wenye hasira kwamba hakutoa hata chembe kimoja cha ardhi kwa mtu yeyote.

Rais wa Misri anayekabiliana na hali ngumu Abdel-Fatah el-Sisi ametetea uwamuzi wake ulosababisha utata wa kukabidhi mamlaka ya visiwa viwili kwa Saudi Arabia na pia kukataa kwamba maafisa wa usalama walihusika na mauaji ya mwanafunzi Mtaliano.

El-Sisi alilihutubia taifa kupitia televisheni kuwahakikishia Wamisri wenye hasira kwamba hakutoa hata chembe kimoja cha ardhi kwa mtu yeyote. Amesema kwamba hawakusalimisha haki yao bali walidumisha haki ya wengine na aliomba suala hilo kuto-zungumziwa tena.

Amewaeleza wananchi kwamba waliachie bunge kujadili suala hilo kwa kuwa ndilo lenye wawakilishi wanaoweza kulijadili kisheria na litaweza kukubaliana ama kukataa shauri hilo. Cairo ilitangaza wiki hii kwamba inapanga kutoa umiliki wa visiwa vya Sanafir na Tiran vilivyo katika Red Sea kwa Saudi Arabia.

XS
SM
MD
LG