Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 16:34

Misri yawaachia huru wanahabari walioshikiliwa


Wanahabari waliokuwa wakishikiliwa nchini Misri, kutoka kushoto ni Baher Mohamed, Mohammed Fahmy, na Peter Greste walipokuwa mahakamani mwaka jana.
Wanahabari waliokuwa wakishikiliwa nchini Misri, kutoka kushoto ni Baher Mohamed, Mohammed Fahmy, na Peter Greste walipokuwa mahakamani mwaka jana.

Mahakama moja nchini Misri, imewaachia waandishi wawili wa habari wa kituo cha televisheni cha Al-Jazeera Alhamisi.

Hiyo ni baada ya kuakhirisha kwa muda kesi yao hadi februari 23, kwa mashtaka ya kulisaidia kundi lililopigwa marufuku nchini humo la Muslim Brotherhood.

Jaji wa mahakama hiyo ya Cairo, aliweka dhamana ya dola za Kimarekani 33,000 kwa Mohammed Fahmy, na hakukuwa na dhamana kwa mwandishi mwenzake Baher Mohammed.

Fahmy alikuwa ana wan chi mbili za Canada, na Misri, kabla ya kuukana uraia wa Misri mwezi huu kwa matumaini ya kuweza kuachiwa huru.

Mwandishi wa tatu wa kituo hicho cha al-Jazeera, raia wa Australia, Peter Greste, aliachiwa na kurudishwa nchini kwake Februari mosi.

XS
SM
MD
LG