Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 05:07

Misri yapata dola milioni 500 kutoka Benki ya Dunia


Mkao makuu ya Benki ya Dunia, jijini Washington DC
Mkao makuu ya Benki ya Dunia, jijini Washington DC

Misri inayo ongoza kwa kuagiza ngano duniani, Jumatano imetangaza kupokea dola milioni 500 kutoka Benki ya Dunia ili kukabiliana na upungufu wa chakula uliotokana na vita vya wasambazaji wake wa kuu wa ngano Russia na Ukraine.

Katia taarifa, waziri wa mahusiano ya kimataifa wa Misri, Rania al-Mashar amesema fedha hizo za benki ya dunia zitasaidia juhudi za serekali kukabiliana na mahitaji ya chakula, na kuwa tayari na hali yoyote kwa wakati ujao.

Hali ya upungufu wa chakula imekuwa katika wasiwasi mkubwa toka Russia kuivamia Ukraine mwishoni mwa mwezi Febuari na kusababisha usumbufu mkubwa katika usafirishwaji wa chakula kwa njia ya bahari.

Kabla ya uvamizi huo, asilimia 85 ya ngano ya Misri ilikuwa ikiagizwa kutoka kwa mataifa hayo mawili ya Ukraine na Russia.

XS
SM
MD
LG