Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:02

Misri yalipiza kisasi mauaji ya raia wake Libya


Wakristo wa Kanisa la Coptic la Misri wakiomboleza wenzao waliouawa Libya
Wakristo wa Kanisa la Coptic la Misri wakiomboleza wenzao waliouawa Libya

Misri ilifanya mashambulizi ya pili ya anga huko mashariki mwa Libya kulipiza kisasi kuuwawa kwa Wakristo 21 wa madhehebu ya Koptik wa Misri yaliyofanywa na wanamgambo wa Islamic State nchini Libya.

Mabomu hayo yaliuwa dazeni ya wanamgambo na raia kadhaa katika ngome ya kundi la Islamic State ya Darna na kwa mujibu wa maafisa wa Libya, ngome hiyo imo kilomita 1,300 mashariki mwa eneo ambalo mauaji ya Wakristo yaliripotiwa kufanyika.

Rais wa Misri Abdel Fattah el- Sissi aliahidi kulipiza kisasi haraka katika hotuba iliyotolewa kwenye Televisheni akiyaita mauaji hayo “kitendo kiovu cha ugaidi.”

XS
SM
MD
LG